Data Privacy Statement TZ-SWAHILI

WATU CREDIT (TANZANIA) LIMITED: SERA YA FARAGHA NA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI

Katao la Haki la Programu Tumizi ya Simu za Mkononi

Taarifa iliyopo kwenye programu tumizi yetu ya simu za mkononi ni kwa ajili ya urahisi wa huduma wa wateja wetu na haipaswi kuchukuliwa kuwa na nguvu kisheria. Programu tumizi ya simu imeandaliwa kwa madhumuni ya kutoa taarifa tu na huenda haijitoshelezi au haioneshi hali ya sasa ya mkopo. Watumiaji wanaarifiwa kwamba taarifa kwenye programu hii haiwezi kutumiwa dhidi ya kampuni ya Watu Credit LTD kwenye shtaka lolote la kisheria. Kwa maelezo ya kina na yenye nguvu kisheria kuhusu hali ya mkopo au masuala mengine yoyote, watumiaji wanahimizwa sana kuwasiliana moja kwa moja na Idara ya Huduma kwa Wateja ya kampuni ya Watu.

Sera ya Faragha na Ulinzi wa Taarifa Binafsi

Sera hii ya Faragha na Ulinzi wa Taarifa Binafsi inakujulisha kuhusu jinsi na kwa malengo yapi Watu Credit Limited, matawi yake na washirika wake katika nchi mbalimbali (wakijulikana hapa kama “Watu” “sisi” au “yetu”) itachakata taarifa zako binafsi na kuelezea haki zako kwenye Sheria ya Faragha na Ulinzi wa Taarifa Binafsi, na Kanuni husika zinazotumika katika nchi tofauti inazofanya kazi. Tumejidhatiti katika kutunza taarifa zako binafsi kwa uwajibikaji, bidii na kutii matakwa yote ya kisheria kwa uadilifu na kuhakikisha usalama wa taarifa zako binafsi.

Kwa madhumuni ya Sera hii ya Faragha na Ulinzi wa Taarifa Binafsi, “taarifa binafsi” inamaanisha taarifa yoyote inayohusiana na mtu aliyetambuliwa au anayetambulika.

  1. Utangulizi 
    1. Watu Credit Limited inafanya kazi katika mazingira ambayo kwa sehemu kubwa yanahitaji data ambazo huchakatwa na hutumia taarifa binafsi ili kutimiza jukumu lake la msingi la kuandaa mikataba ya mikopo kwa umma inayofadhiliwa na mali. 
    2. Kampuni ya Watu inaheshimu faragha ya watu na tunatambua unyeti wa taarifa binafsi tunazopewa na wateja na wafanyakazi wetu na watu wengine. Ni jukumu letu -kwa kutumia njia yenye tija na inayofaa – kuchakata na kulinda taarifa zote binafsi kwa mujibu wa sheria na kanuni husika za ulinzi wa taarifa binafsi. 
    3. Sera hii ya Faragha na Ulinzi wa Taarifa Binafsi inafafanua taarifa binafsi tunazokusanya, jinsi tunavyozishughulikia, kwa madhumuni gani na ni nani tunaweza kufichua kwake katika muktadha wa mahusiano yetu. Pia inaelezea jinsi Watu inavyoshughulikia taarifa zako inazozimiliki na mfumo wa udhibiti ambao Watu imeanzisha ili kulinda taarifa zako. Zaidi ya hayo, Sera hii inajumuisha taarifa kuhusu haki zako kuhusiana na uchakataji wa taarifa zako binafsi. 
    4. Tunaweza kurekebisha mara kwa mara Sera hii ya Faragha na Ulinzi wa Taarifa Binafsi ili kuendana na mabadiliko ya sheria au desturi za kibiashara. Tutaweka mabadiliko yote ya taratibu za Maombi, Makubaliano na Sera husika kwenye tovuti yetu. Toleo jipya la Sera yetu litachukua nafasi na kufuta matoleo yote ya awali, isipokuwa kama imeelezwa vinginevyo na litapatikana ili kufikisha ujumbe kwa wote. Tutakujulisha kuhusu mabadiliko muhimu ya Sera hii kupitia arifu itakayowekwa kwenye tovuti yetu au kupitia njia nyingine yoyote inayofaa ya mawasiliano.
    5. Sera yetu ya Faragha na Ulinzi wa Taarifa Binafsi inatumika kwa wageni wanaotembelea ofisi zetu au tovuti yetu na pia wateja, wasambazaji, mawakala, wafanyakazi na wadau wetu wote. 
  2. TAFSIRI YA MANENO MUHIMU 
    1. Maneno Sisi/yetu/ yanamaanisha Watu Credit (Tanzania) Limited (Kampuni na matawi yake na washirika wake).
    2. Afisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi ni mtu ambaye kampuni imemteua au kumpatia jukumu la kusimamia uzingatiaji wa Sheria na Kanuni mbalimbali za Faragha na Ulinzi wa Taarifa Binafsi.
    3. Ukusanyaji wa Taarifa unamaanisha kukusanya taarifa kunakohusiana na wewe/mtumiaji.
    4. Taarifa binafsi inamaanisha taarifa kukuhusu ambayo inakutambulisha moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kama vile jina, namba ya utambulisho, taarifa ya mahali, utambulisho wa mtandaoni au kwa kutumia kielelezo kimoja au zaidi mahususi kwa utambulisho wa kimwili, kifiziolojia, maumbile, kiakili, kiuchumi, kiutamaduni au kijamii wa mtu. Taarifa binafsi tunazokusanya zitategemea aina ya mahusiano yaliyopo kati yetu. Tunaweza kukusanya, kutumia, kuhifadhi na kuhamisha aina tofauti za taarifa zako binafsi au watu unaohusiana nao.
    5. Kuchakata kunamaanisha kufanyia kazi taarifa zako binafsi iwe kwa njia ya kujiendesha, kama vile: kukusanya, kurekodi, kupangilia au kupangilia upya; Kuhifadhi, kutohoa au kubadili; Kurekebisha, kushauriana au kutumia; Kufichua kwa upelekaji, usambazaji, au vinginevyo kuweka mazingira ya upatikanaji; Mfungamano au mchanganyiko, kuzuia, kufuta au kuharibu.
    6. Taarifa nyeti binafsi ni taarifa inayoelezea asili au kabila lako, mlengo wa kisiasa, uanachama wa kitaaluma, na uchakataji wa taarifa za kijenetiki, na bayometriki kwa madhumuni ya kumtambua mtu, taarifa za afya au jinsia yake.
    7. Mtu wa tatu/mtu mwingine – inamaanisha binadamu au mtu kisheria, taasisi ya umma au binafsi, wakala au chombo kingine, isipokuwa wewe/mteja na kampuni ya Watu, ambaye ameidhinishwa na Watu kuchakata taarifa zako binafsi.
    8. Wewe/ Wako inamaanisha:
      1. Mtu yeyote ambaye amepakua na kutumia programu tumizi zetu zozote za simu.
      2. Mtu yeyote ambaye amesaini Mkataba na Watu.
      3. Mfanyakazi yeyote ambaye ameajiriwa na Watu.
      4. Wakala yeyote, muuzaji na/au mfanyabiashara ambaye ana makubaliano na Watu na anatambuliwa kama mfanyabiashara au wakala kwa mujibu wa sheria au Kanuni husika.
      5. Mgeni yeyote ambaye ni mtu (ikiwa ni pamoja na mkandarasi/mkandarasi mdogo au mtu wa tatu) ambaye atafika kwenye jengo/ofisi za Watu.
      6. Msambazaji/mtoa huduma yeyote mwenye mkataba na Watu.
      7. Wakili/mwanasheria yeyote wa nje ambaye ana makubaliano ya kutoa huduma kwa Watu.
      8. Mtoa huduma mwingine yeyote au taasisi ya kifedha ambayo ina makubaliano na Watu.
    9. “Kuchakata” kwa ujumla kunamaanisha kushughulikia, kukusanya, kutumia, kubadilisha, kuunganisha, kuhusianisha, kupangilia, kusambaza, kuhifadhi, kulinda, kurekebisha, kufichua, kufuta, kuhifadhi, kuharibu, au kutupa taarifa zako binafsi.
  3.  Kanuni za jumla za Watu za kulinda taarifa binafsi ni:
    1. Tuna uwazi kuhusu jinsi tunavyotekeleza sheria husika ya ulinzi wa taarifa binafsi.
    2. Tunadhibiti ukusanyaji na uchakataji wa taarifa binafsi kama sheria inavyotaka. Taarifa tunayokusanya kuhusu wewe ni kwa madhumuni maalum na halali na haitachakatwa zaidi kwa namna ambayo haiendani na madhumuni hayo.
    3. Tunachakata taarifa nyeti binafsi ikiwa tu uchakataji husika una misingi ya wazi na inayoelezeka kisheria.
    4. Tunachukua maelezo kuhusu watu binafsi ili kufikia madhumuni ya uchakataji. 
    5. Tunawajulisha watu binafsi aina ya taarifa binafsi tunazokusanya na jinsi taarifa hizi zitahifadhiwa na kutumiwa.
    6. Tunashughulikia taarifa binafsi kwa usiri mkubwa na tunachukua hatua stahiki za kiufundi na kitaasisi ili kulinda taarifa binafsi dhidi ya upotevu au ufikiaji na uchakataji kinyume cha sheria.
    7. Tunahifadhi taarifa binafsi kwa muda mahsusi tu ili kutimiza madhumuni ambayo kwayo zilikusanywa, au kwa kadri matakwa ya sheria mahalia zinaelekeza.
    8. Ikiwa uchakataji wetu wa taarifa binafsi unaweza kuhatarisha haki na uhuru wa watu binafsi, tutafanya tathmini ya athari za ulinzi wa taarifa na, ikibidi, kuchukua hatua zinazofaa za kiusalama kwa kuzingatia maelekezo ya Ofisi ya Kamishna wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini Tanzania na katika Nchi nyingine yoyote ambayo tunaendesha shughuli zetu. 
    9. Mifumo na taratibu zetu zinasaidia ulinzi wa taarifa binafsi. Tunatunza nyaraka zinazoonesha kwamba mifumo na taratibu zetu zinafanya kazi kama ilivyokusudiwa.
    10. Tunapotumia watu wengine kuchakata taarifa binafsi, tunaweka wajibu wa kimkataba kulinda taarifa husika.
  4. Kwa nini tunakusanya taarifa zako binafsi?

Tunakusanya taarifa zako binafsi kwa madhumuni yafuatayo:

  1. Ikiwa tunahitaji kutimiza matakwa ya mkataba ambao tunakaribia kuingia au tumeingia na wewe.
  2. Kutathmini ikiwa unasifa za kupata huduma na bidhaa zetu.
  3. Ikiwa umetupatia idhini ya kutumia taarifa zako binafsi.
  4. Pale ambapo tunahitaji kuzingatia au kutimiza matakwa ya kisheria au udhibiti, na kujilinda au kuwalinda wateja wetu dhidi ya ulaghai.
  5. Ikiwa tunahitaji kulinda masilahi yako muhimu na mtu wa tatu (kwa mfano, wakati wa kuwasiliana na wanufaika/mdhamini wako waliotajwa na Mkataba.
  6. Ikiwa ni muhimu katika kulinda masilahi yetu halali (au ya mtu wa tatu) kama vile kutunza kumbukumbu zetu, kukuza, kutathmini, na kuboresha huduma zetu, kufanya tathmini ya hatari, kuboresha usimamizi na ushiriki wa wateja wetu pamoja na kuzingatia matakwa yetu ya Jua Mteja Wako (JMW).
  7. Kuanzisha, kutekeleza au kutetea haki zetu za kisheria kama vile tunapokabiliwa na madai yoyote ya kisheria au ambapo tunataka kufuatilia haki zetu kisheria.
  8. Kutangaza bidhaa na huduma mpya (tafadhali kumbuka kwamba ikiwa hutaki kupokea taarifa zetu za masoko unaweza kujiondoa kwa kuwasiliana nasi wakati wowote).
  9. Ili kukutumia arifu (notisi) muhimu kama vile mabadiliko ya masharti, vigezo na sera zetu, ofa zozote, mapunguzo, salio la mkopo au jambo lisilo la kawaida kuhusiana na Mkataba kati yetu.
  10. Ikiwa unaomba ajira katika kampuni ya Watu au tunagundua kuwa una sifa za kuajiriwa, tunaweza kutumia taarifa zako binafsi kutathmini sifa za kuajirika kwako na kuwasiliana nawe kuhusu fursa ya ajira.
  11. Tunapopokea taarifa zako binafsi kutoka kwa mtu wa tatu, tunaweza kuzitumia kuthibitisha taarifa uliyotupatia kwa madhumuni ya kuzuia ulaghai.
  12. Ili kutuwezesha kukusajili kwenye huduma zetu na kuthibitisha utambulisho wako na uwezo wa kutumia huduma zetu.
  13. Ili kushughulikia ulaghai au kero za kiusalama, au kuchunguza malalamiko au tuhuma za ulaghai au kuvunja sheria.
  14. Kufuatilia na kupembua majukwaa yetu kwa madhumuni ya usimamizi wa mfumo, uendeshaji, upimaji na kutoa msaada.
  15. Kushirikiana na, kujibu maombi kutoka kwa, na kuripoti miamala na/au shughuli nyingine kwa serikali, taasisi ya kodi au vyombo vya udhibiti, au mawakala wao au washirika, mahakama au mtu wa tatu. 
  1. Ni taarifa za nani tunazokusanya?

Tunakusanya taarifa zako binafsi kwa sababu wewe ni mteja wetu au tuna uhusiano mwingine wa thamani. 

  1. Tunakusanyaje taarifa zako binafsi?

Tunakusanya taarifa zako binafsi ukiwa unajua na kwa idhini yako. Tunaweza kukusanya taarifa zako binafsi kwa kutumia njia yoyote kati ya hizi: (tafadhali kumbuka kuwa orodha hii sio timilifu):

  1. Kutoka kwako binafsi, kama vile wakati wa kuingia mkataba na sisi kama mteja au mkandarasi, 
  2. Kwa kutembelea ofisi zetu au tovuti yetu, 
  3. Kwa kupakua programu tumizi zetu za simu na kujisajili,
  4. Kwa kujisajili mwenyewe kwenye orodha ya mawasiliano yetu, 
  5. Kujiandikisha kwa ajili ya tukio, kuomba kazi,
  6. Kutoka vyanzo vingine, kama vile washirika wa kibiashara,
  7. Kwa kutembelea tovuti yetu. Tunakusanya taarifa binafsi kwa kutumia vidakuzi na teknolojia kama hizo. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu hili kwenye kipengele cha sera ya tovuti na vidakuzi,
  8. Kutoka kwenye vyanzo vinavyofikiwa na umma ikiwa ni pamoja na: 
  9. Taarifa za utambulisho na mawasiliano kutoka majukwaa ya kidigitali ya Serikali ya Tanzania ya Huduma Jumuishi za Usajili wa Wananchi Mtandaoni kama inavyotumika katika nchi nyingine yoyote ambapo taarifa zako zimekusanywa.
  10. Taarifa za utambulisho na mawasiliano kutoka vyanzo vinavyofikiwa na umma kama vile Wakala wa Usajili wa Kampuni na Biashara.
  11. Taarifa za kifedha na miamala kutoka rejista za ardhi, hifadhidata za kisekta kama vile taasisi za kurejelea mikopo, mashirika ya kuzuia ulaghai na watoa huduma za kiufundi, malipo na wakala wa fedha.
  12. Wataalamu wa afya na hospitali.
  13. Mitandao ya kijamii- Ikiwa wewe ni mtu anayeweza kuajiriwa na kampuni ya Watu, tunaweza kuwa tumepokea taarifa zako binafsi kutoka kwa mtu wa tatu kama vile wakala wa ajira au tovuti za nje.
  14. Kutoka kwa mtu binafsi.
  15. Kutoka kwa mtu mwenye madai au maombi, na akajumuisha taarifa zako ambazo zinahusiana na madai au maombi yake.
  16. Kutoka kwa wanafamilia wanapoulizia mali au kukujumuisha kama ndugu wa karibu kwenye maombi yao.
  17. Rekodi kutoka kwenye Mfumo wa Kamera za Usalama (CCTV). Vifaa vya CCTV vimewekwa katika maeneo ya kimkakati kwenye ofisi za Watu ili kuwa na mazingira salama.

Kwa kuchagua kuingiliana nasi kwa njia yoyote iliyoainishwa chini ya kifungu cha 6.0 hapo juu, utakuwa ukifanya hivyo ukifahamu fika na kukubali kwamba tutakusanya na kuchakata taarifa zako binafsi. Kwa kukubali, unaturuhusu kukusanya, kuchakata, kuhifadhi, kufichua na kuhamisha taarifa zako kama ilivyoelezwa chini ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na kanuni zake.

  1. Ni aina gani ya taarifa binafsi tunakusanya?

Taarifa binafsi ambazo tunachakata zinaweza kujumuisha:

  1. Taarifa ya utambulisho kama vile jina, tarehe na mahali pa kuzaliwa, namba ya kitambulisho cha kitaifa, namba ya hati ya kusafiria, Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN), picha, hali ya ndoa, cheo, uraia, jinsia, na sahihi yako.
  2. Taarifa za mawasiliano kama vile barua pepe, anwani ya posta, anwani ya mahali, anwani ya makazi, na namba ya simu.
  3. Taarifa ya kifedha kama vile maelezo ya akaunti ya benki, maelezo ya kadi ya malipo, taarifa za miamala ya mtandaoni, mapato, historia ya mkopo, uwezo wa kukopesheka, taarifa za benki, taarifa za kulipwa au kufanya malipo na maelezo mengine ya bidhaa na huduma ulizopata kupitia kwetu.
  4. Taarifa juu ya ushiriki wako katika suala linalosababisha madai.
  5. Taarifa kuhusu aina ya biashara yako na mali za kibiashara.
  6. Taarifa za ajira yako kama vile jina la mwajiri, cheo chako na anwani ya taasisi husika.
  7. Taarifa binafsi za Watoto kama vile jina, tarehe ya kuzaliwa na jinsia.
  8. Taarifa nyeti binafsi kama vile hali ya ndoa, taarifa za mali, hali ya afya na maelezo ya familia (kama vile ndugu wa karibu na wanufaika).
  9. Taarifa za masoko na kupashwa habari ikiwa ni pamoja na mahitaji yako katika kupokea taarifa za masoko na kupashwa habari na sisi.
  10. Taarifa za mtandaoni wakati wowote tembelea tovuti yetu na programu tumizi za simu kama vile vidakuzi, taarifa za kuingia katika mfumo wa kikompyuta, anwani ya kompyuta (anwani ya intaneti ya kompyuta yako), aina na toleo la kivinjari, Mtoa huduma wa mtandao au mfumo wa uendeshaji kompyuta, jina la kikoa, muda uliotembelea mfumo, kupekua kurasa na mahali husika.
  11. Taarifa za kijiografia za mahali- Tunaweza kuomba kupata ruhusa ya kufuatilia taarifa za mahali kutoka kwenye kifaa chako cha mkononi, iwe muda wote au unapotumia programu tumizi zetu za simu, ili kutoa huduma fulani zinazoendana na mahali husika. Ikiwa ungependa kubadili ufikiaji au idhini ulizotoa, unaweza kufanya hivyo katika sehemu ya mpangilio ya kifaa chako.
  12. Ufikiaji wa Kifaa cha Mawasiliano cha Mkononi- Tunaweza kuomba ufikiaji au ruhusa ya kufikia vitumizi fulani kwenye kifaa chako cha mawasiliano, ikiwemo ujumbe mfupi na vitumizi vingine. Ikiwa ungependa kubadili ufikiaji au idhini ulizotoa, unaweza kufanya hivyo katika sehemu ya mpangilio ya kifaa chako.
  13. Taarifa za Kifaa cha Mawasiliano cha Mkononi- Tunakusanya papo kwa papo taarifa za kifaa husika (kama vile namba ya utambulisho ya kifaa cha mkononi, modeli, na mtengenezaji), mfumo wa uendeshaji kompyuta, maelezo ya toleo na usanidi wa mfumo, namba za utambulisho wa kifaa na programu tumizi, aina na toleo la kivinjari, modeli ya vifaa vya mtoa huduma za mtandao na/au mtoa huduma za simu, na anwani ya Itifaki ya Mtandao (au seva mbadala). Ikiwa unatumia programu zetu tumizi, tunaweza pia kukusanya taarifa kuhusu mtandao wa simu unaotumiwa na kifaa chako cha mkononi, mfumo wa kikompyuta wa uendeshaji wa kifaa chako cha mkononi au jukwaa husika, aina ya kifaa cha mkononi unachotumia, utambulisho wa kipekee wa kifaa chako cha mkononi na taarifa kuhusu vipengele vya programu zetu tumizi ulivyofikia.
  14. Arifu za mara kwa mara- Tunaweza kukuomba uturuhusu tukutumie arifu za mara kwa mara kuhusu akaunti yako ya mteja au vipengele fulani vya programu tumizi. Ikiwa ungependa kujiondoa kwenye aina hizi za kupashana habari, unaweza kuzima kipashio husika kwenye sehemu ya mpangilio wa kifaa chako cha mawasiliano. 

Ikiwa kuna hitaji stahiki la taarifa kuhusu watu wengine wanaokuhusu, tunaweza kukuomba utoe taarifa kuhusu watu hao. Ikiwa unatoa taarifa kuhusu mtu mwingine, tunatarajia uhakikishe kwamba mtu huyo anajua kwamba unafanya hivyo na ameridhia taarifa zake husika kutolewa kwetu. Inaweza kuwa vyema kuwaonesha Sera hii ya faragha na ulinzi wa taarifa binafsi na ikiwa wana dukuduku lolote, tafadhali wasiliana nasi.

  1. Ni nani tunampatia taarifa zako binafsi?
    1. Tunaweza kutoa taarifa zako binafsi kwa makampuni mengine na kampuni tanzu ndani ya Kundi la Makampuni ya Watu kwa ajili ya kuchakata taarifa zako binafsi kulingana na madhumuni husika. Taarifa zako binafsi zinaweza pia kutolewa kwa washirika wa Watu wanaoaminika, kama vile wauzaji, wazalishaji na wahusika wengine walioorodheshwa hapa chini, ili kufikia madhumuni husika. Tutahakikisha kwamba ulinzi unaofaa wa kimkataba unawekwa na kutekelezwa ili kuhakikisha usalama wa taarifa zako binafsi wakati wa ufichuaji kwa mtu wa tatu. 
    2. Kwa kuzingatia haki zako na sheria zinazotumika, tunaweza kutoa taarifa zako binafsi kwa watu wengine walioorodheshwa hapa chini:
      1. Mamlaka za umma au serikali inapohitajika kufanya hivyo kisheria, maslahi ya umma, usalama wa taifa, kanuni, mchakato wa kisheria au kutekeleza ombi la serikali.
      2. Watu au taasisi ambazo umetuomba waziwazi tuzipatie taarifa zako binafsi.
      3. Ndugu zako, walezi au watu wawakilishi wako kama una ulemavu au kwa madhumuni ya kumalizana na wanufaika wako.
      4. Kampuni za bima, mdalali wa bima, bima mtawanyo, na mawakala wa huduma za bima.
      5. Washauri wetu wa kitaalamu kama vile wakaguzi mahesabu, washauri kodi, bima, mdalali wa bima, watoa huduma za afya, wanasheria ambao hufanya kazi kwa niaba yetu au yako, au ambao wanawakilisha mtu wa tatu.
      6. Taasisi na wataalamu wa afya ikiwa tutahitaji tathmini na taarifa zako za kiafya kwa madhumuni maalum.
      7. Mashirika ya kukusanya madeni, mashirika ya kumbukumbu za mikopo, mashirika ya kugundua ulaghai na mashirika mengine ambayo tuna mkataba nao wa utoaji huduma.

Ikiwa taarifa binafsi inapelekwa nje ya nchi zilipo kusanywa au kuchakatwa, hatua zinazofaa zitachukuliwa ili kuhakikisha ulinzi wa taarifa zako binafsi.

  1. Tunahifadhije taarifa zako binafsi?

Kampuni ya Watu hudumisha ulinzi unaofaa wa kiufundi na kitaasisi dhidi ya uchakataji usioidhinishwa, upotevu, madhara, au uharibifu wa bahati mbaya wa taarifa binafsi.

  1. Tunahifadhi taarifa zako binafsi kwa muda gani?
    1. Tutahifadhi taarifa zako binafsi kwa kadri iwezekanavyo ili kutimiza kusudi la ukusanyaji tu, ikiwa ni pamoja na kukidhi matakwa ya kisheria, udhibiti, kodi, uhasibu au kutolea taarifa.
    2. Tunaweza kuhifadhi taarifa zako binafsi kwa muda mrefu ikiwa uhifadhi huo:
      1. umeidhinishwa au ni takwa la kisheria.
      2. muhimu kwa madhumuni ya kisheria.
      3. kumeidhinishwa au kukubaliwa na wewe.
      4. ni muhimu kwa madhumuni ya kujibu malalamiko au ikiwa tunaamini kuna uwezekano wa kuwepo kesi kutokana na uhusiano wetu na wewe.
      5. kwa madhumuni ya historia, takwimu, uandishi wa habari, fasihi na sanaa au utafiti.
  2.  Tunalindaje taarifa zako binafsi?
    1. Tumechukua hatua zinazofaa za kiusalama ili kuzuia taarifa zako binafsi kupotea kimakosa, kutumiwa au kufikiwa kwa njia isiyoidhinishwa, kubadilishwa au kufichuliwa. 
    2. Zaidi ya hayo, tunawekea kikomo ufikiaji wa taarifa zako binafsi kwa wafanyakazi, mawakala, wakandarasi na wahusika wengine ambao wana biashara na wanahitaji kujua. Watachakata tu taarifa zako binafsi kwa maelekezo yetu, na wana wajibu wa kutunza siri.
  3. Haki zako kama Mhusika wa Taarifa Binafsi ni zipi na unawezaje kuzitumia?

Una haki ya:

  1. kupewa taarifa kuhusu na ufikiaji wa taarifa zako binafsi;
  2. kurekebisha taarifa zako binafsi;
  3. kufuta taarifa zako binafsi (‘haki ya kusahaulika’);
  4. kuweka masharti juu ya uchakataji wa taarifa zako binafsi;
  5. kupinga uchakataji wa taarifa zako binafsi;
  6. kupokea taarifa zako binafsi katika mpangilio mzuri, wa kawaida na unaosomeka kwenye mashine na, pale ambapo inawezekana kiufundi, taarifa zako binafsi zinapopelekwa kwenye shirika lingine;
  7. kupeleka malalamiko katika Ofisi ya Kamishna wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini Tanzania na kwa Mdhibiti katika nchi nyingine yoyote ambapo kuna ukiukwaji au tukio limetokea kuhusu utunzaji wa taarifa zako.

Ili kutumia haki zako, tafadhali tuma barua pepe kwenda: [email protected]

Kunaweza kuwa na sababu zinazozuia haki zako, haswa ikiwa uchakataji wa taarifa zako binafsi kunahitajika ili kutimiza wajibu wetu kisheria au udhibiti.

  1. Kanuni Zetu za Usalama
    1. Tumejidhatiti na tunalazimika kutekeleza tahadhari zote muhimu za udhibiti ili kulinda ufikiaji wa taarifa zako binafsi.
    2. Pale ambapo wahusika wengine wanahitaji kuchakata taarifa zako binafsi kuhusiana na madhumuni yaliyowekwa katika Sera hii na kwa matakwa mengine ya kisheria, tunahakikisha kwamba wanalazimika kimkataba kutekeleza kanuni muhimu za kiusalama.
    3. Matumizi yote ya tovuti yetu yanalindwa kupitia usimbaji fiche salama kulingana na viwango bora vya kimataifa.
  2. Je, tunakusanya taarifa binafsi kutoka kwa watoto?
    1. Hatukusanyi taarifa kwa makusudi kutoka au kufanya shughuli za masoko kwa watu chini ya umri wa miaka 18, ambao pia hujulikana kama vichanga/watoto.
    2. Hatuombi kwa makusudi taarifa kutoka au kutangaza bidhaa kwa watoto chini ya umri wa miaka 18. Kwa kutumia Huduma zetu, unajibainisha kwamba una umri, angalau, wa miaka 18 au kwamba wewe ni mzazi au mlezi wa mtoto kama huyo na unakubali mtoto/mtegemezi wako kutumia Huduma zetu. Ikiwa tutafahamu kwamba taarifa binafsi kutoka kwa watumiaji walio chini ya umri wa miaka 18 zimekusanywa, tutasitisha akaunti ya mtumiaji na kuchukua hatua zinazofaa za kufuta taarifa binafsi husika mara moja kutoka kwenye rekodi zetu. Ikiwa unafahamu taarifa yoyote, ambayo huenda tumekusanya kimakosa kutoka kwa watoto chini ya umri wa miaka 18, tafadhali wasiliana nasi kupitia [email protected]
  3. Matumizi binafsi ya barua pepe na taarifa kuhusu kuangalia barua pepe
    1. Mifumo yetu ya mawasiliano na taarifa ni kwa ajili ya matumizi ya kibiashara tu. Hata hivyo, tunatambua kwamba wafanyakazi wetu mara kwa mara hutumia mifumo husika ya mawasiliano kwa matumizi binafsi. 
    2. Matumizi binafsi ni pamoja na kutuma au kupokea barua pepe binafsi ndani au nje ya kampuni ya Watu. Ingawa wafanyakazi wetu wanabanwa na sera kali za matumizi na usalama, hatutowajibika kwa maudhui yoyote yatokanayo na wafanyakazi wetu kufanya matumizi binafsi ya barua pepe na mifumo yetu ya mawasiliano. 
    3. Tafadhali kumbuka kwamba tunaweza kuzuia, kukagua na kufuta mawasiliano yoyote yaliyoandaliwa, hifadhiwa, kutumwa, au kupokea kwa kutumia mifumo yetu, kwa mujibu wa Sheria yoyote iliyopo.
  4. Mawasiliano

Tumeteua afisa ulinzi wa taarifa binafsi ambaye atajibu maswali yote kuhusiana na Sera hii ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi. Ikiwa una swali au dukuduku lolote kuhusu matumizi ya taarifa zako binafsi au kuhusu Sera hii ya ulinzi wa taarifa binafsi, ikiwa ni pamoja na maombi yoyote ya kutumia haki zako za sheria, tafadhali wasiliana nasi kwa kutumia maelezo yaliyowekwa hapa chini:

Barua pepe:  [email protected]

Anwani ya posta: S.L.P 76536,

Anwani ya mahali: Ghorofa ya 1, Barabara ya Golden Heights Chole, Masaki, Dar es Salaam

Namba ya simu: 0800 750 228



Sera hii Imeanza Kutumika Rasmi Tarehe: 14 Februari 2024

Sera hii ya Faragha na Ulinzi wa Taarifa Binafsi iliyosasishwa mara ya mwisho tarehe (14 Februari 2024)




Get a Logbook loan with Watu Gari