Watu Simu inakuletea dunia kiganjani!

Kianzio kidogo

Jipatie mkopo wa simu leo kwa kianzio kidogo tu!

Malipo rafiki

Marejesho nafuu kila wiki, kwa wiki 52 tu.

Vigezo rahisi

Masharti na vigezo rahisi kabisa, njoo na vigezo vyote upate mkopo wako chap chap.

Maswali Yanayoulizwa Mara Kwa Mara

Watu Simu inatoa mikopo nafuu na rahisi, kwa aina mbalimbali za simu janja ndani ya soko la Tanzania.

Watu Simu inatoa mikopo ya simu janja  za aina ya Samsung Galaxy. Simu hizo  zina waranti ya miezi 24.

 • Kitambulisho halisi kati ya NIDA, kura au leseni ya udereva.
 • Usiwe na mkopo mwingine na Watu.
 • Uwe na umri kuanzia miaka 18.
 • Taarifa za simu ya mtu wa karibu (lazima awe anapatikana kwenye simu kwa ajili ya uhakiki).
 • Kianzio cha malipo ya awali ya simu ulioichagua.
 1. Tembelea duka ambalo huduma ya Watu Simu inapatikana.
 2. Chagua simu yoyote ya aina ya Samsung Galaxy ambayo imehakikiwa na Watu.
 3. Pata ruhusa ya awali kuhusu maombi yako.
 4. Lipa malipo ya awali elekezi.
 5. Subiri hatua za uhakiki zikamilike.
 6. Baada ya uhakiki kukamilika, simu itawashwa na utaweza kuondoka na simu yako.

Zifuatazo ni aina ya simu zinazopatikana kwa mkopo kupitia Watu Simu;

 • Samsung Galaxy A03 Core
 • Samsung Galaxy A04
 • Samsung Galaxy A04S
 • Samsung Galaxy A04E
 • Samsung Galaxy A14
 • Samsung Galaxy A24
 • Samsung Galaxy A34
 • Samsung Galaxy A54

Namba ya malipo: 650880

Akaunti namba: Namba ya simu ya mteja.

Endapo hukufanya marejesho yako ya wiki kama ilivyoainishwa kwenye mkataba wa mkopo, simu yako itazimwa. Unaweza kufanya marejesho unayodaiwa kupitia namba ya kampuni 650880 ili kufungua simu yako.

Endapo umefanya marejesho yako kwa wakati na simu yako imefungwa, inawezekana simu yako haikuwa kwenye mtandao kwa muda mrefu hivyo basi kwa msaada zaidi tupigie huduma kwa wateja bure: 0800 750 228 kupata msaada wa haraka.

Kwa tatizo lolote la kiufundi, tafadhali wasiliana na Watu Simu huduma kwa wateja: 0800 750 228 Wahudumu wetu watakushauri kituo  cha matengenezo kilichopo karibu nawe ili uweze kupata huduma ya ukaguzi/matengenezo ya simu yako.

Tafadhali wasiliana na huduma kwa wateja kuhusu simu iliyoibiwa/kupotea. Hakikisha una namba ya IMEI ya simu tajwa, kisha toa taarifa kwenye kituo cha polisi karibu yako ili upate nakala ya taarifa ya upotevu wa simu yako na uwasilishe taarifa hizo kwa huduma kwa wateja wa Watu Simu kupitia namba 0800 750 228 bure.

Kama umenunua Samsung Galaxy A13 au A23, simu yako imesajiliwa kwenye matengenezo ya mara moja ya kioo chako.

Endapo utahitaji huduma hii tafadhali piga huduma kwa wateja 0800 750 228.

Ili uweze kupata huduma hii, pia utalipia kiasi kidogo cha matengenezo kwenye service center za Samsung kama utakavyoelekezwa.

Una maswali zaidi?

Iwapo unahitaji kufika ofisi ya Watu Simu iliyo karibu zaidi au unataka maelezo zaidi kuhusu kupata mkopo  wa simu yako, wasiliana na timu yetu ya huduma kwa wateja.

Ongea nasi:

Chat na timu yetu ya huduma kwa wateja.

Ungana nasi:

Tutumie barua pepe

Get a Logbook loan with Watu Gari